Facebooktwitterredditpinterestlinkedintumblrmail

degrowth_conference_budapest_2016

Budapest itawakaribisha wageni kwa mkutano wa tano wa kimataifa ya Degrowth kwenye chuo kikuu cha Corvinus (kati ya tarehe 30 Agusti na 3 Septemba 2016). Mkutano huu utahushisha wanaojishughulisha na Degrowth wanaojulikana kwa sasa pamoja na wahadhiri na wasikilizaji kutoka nchi ya Hungary na eneo zingine mbali mbali. Wakati huohuo Budapest itakuwa pahali pa kukaribisha Wiki ya Degrowth ya kwanza ambapo wahamasishaji watendaji wa degrowth vile vile weledi na watengenezaji wa sera wengi watafanywa kuwa maarufu.

Degrowth ni mabadiliko ya mawazo inayotukumbusha kuwa maendeleo yasio na kikomo kwa sayari iliyo na kikomo si jambo la kuendelezwa wala ya kufaa. Degrowth inaondoa uwongo uliowekwa kuwa maendeleo ni ufumbuzi mkuu wa kizuizi kilichoelekezwa na mifumo yetu ya jamii. Hii mabadiliko ya mawazo inajaribu kuelewa kukutana kwa hali za hatari tunazopitia na inajadili kuwa mambo haya yana uhusiano kati yao. Mabadiliko ya mawazo ya Degrowth inajaribu kubuni njia shwari na zenye kuunga mkono demokrasi ili kuwe na wingi wa haki ya mashirikiano na mazingira, ustawi, kazi zilizo za maana, ukombozi, watu wachangamfu na wanaojitawala.

Budapest itawakaribisha wageni kwa mkutano wa tano wa kimataifa ya Degrowth kutoka tarehe 30 Agusti mpaka tarehe 3 Septemba 2016. Baada ya mkutano wa kimataifa uliofanyika Paris 2008, ule wa Barcelona 2010, ule wa Venice 2012 na ule wa Leipzig 2014, mkutano huu, ambao unasisitiza maendeleo ya ikolojia na usawa katika mashirikiano, itafanyika katika chuo kikuu cha Corvinus iliyo Budapest.

Awali ya yote, mkutano huu ni pahali wanapokutana watafiti wa kitaaluma wanaojulikana kutoka kwote duniani. Baada ya kila miaka miwili kukutana kwao inawapa sababu ya kujadiliana juu ya maendeleo mapya katika uwanja wa kitaaluma ya utafiti mpya yenye kuingiliana. Wanasisitiza juu ya suala zinazohusika na uvunjaji wa mipaka ya mazingira na miundo msingi wa kiuchumi kutofaulu kuandaa maisha yenye heshima kwa mfumo wa jamii. Jumuia ya wana sayansi pia litaathiriana na weledi muda wote wa mkutano makusudi kuelezea kwa ufasaha kibadala chenye uwezo wa kujitegemea badala ya mitindo yanayokabiliwa na wengi ya kijamii na kiuchumi.

Katika mkutano huu, muda utadhihirishwa kwa umma. Budapest itakuwa chanzo cha kuanzisha jambo jipya, linaloitwa Degrowth Week, ambalo litabuni jukwaa mpya ya bidii ya kiutendaji na warsha nyingi, ubia katika mambo mapya yanayoanzishwa na mahali maalum, kushiriki katika majadiliano na hoja zilizo miongoni mwa washika madau, na mipango ya shughuli za utamaduni, usanii na vitu vwa kubuni kote jijini. Wakati wa majira ya kuchipua ya mwaka wa 2016, watu wote wataalikwa kusaidia waandalizi kutengeneza matokeo ya wiki ya Degrowth.

Degrowth si suala jipwa kabisa hapa Hungary. Mkutano huu utasisitizia kazi ya mhangaria mwenye akili na mashuhuri Karl Polanyi na hasa kazi yake ya msingi “The Great Transformation”. Kipindi cha miaka kumi baada ya uchapishaji wa huu kipande cha msingi, degrowth iliingia tena Hungary mwaka wa 2011 na utafsiri wa kitabu cha Serge Latouche “Farewell to Growth” kwa lugha ya kihangaria. Tangu wakati huo degrowth ni hoja iliyojadiliwa kwa nguvu na uchapishaji wa vitabu kadhaa, makala, pamoja na maandalizi ya majadiliano ya umma na kushiriki kwenye warsha nyingi. Hii pia inashawishi maendeleo ya chanzo cha vitendo vya mahali palepale kama vile Cyclonomia au Cargonomia.

Jiunge nasi hapa Budapest!

The Budapest Degrowth Conference organisation team
https://budapest.degrowth.org/
contact@budapest-degrowth.org
Translated by: Linda Ouma.